Na George Mganga
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga amewacharukia Azam TV akiwalaumu kutokutangaza kitendo cha Kelvin Yondani kutemewa mate wakati wa mchezo wa Yanga SC dhidi ya Singida United uliofanyika Uwanja wa Namfua.
Mkemi amehoji iweje Azam TV hawajatilia nguvu kutangaza tukio hilo huku akieleza kuwa wao na Simba baba yao ni mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mkemi amewauliza Azam TV kuwa Camera zao zilikuwa wapi wakati tukio hilo linafanyika? Ina maana hawakuliona hilo?
"Kujisaidie ajisaidie kuku tu, Haji Manara, TFF na Azam TV hii haikushabikiwa wala hamkuitangaza kwakuwa nyinyi na Simba baba yenu mmoja, Azam TV hii kamera zenu haikuona siyo?" aliandika Mkemi.
Hata hivyo, Mkemi ameweka clip ya Azam TV inayoonyesha Yondani akiwa na mate eneo la sikio lake, akimtuhumu Batambuze kumtemea.
Baadhi ya wachangiaji wamekuwa wakimhoji Mkemi kwa hatua yake hiyo kwamba vipi anawalaumu Azam TV huku akitumia video ya Azam TV kuonyesha Yondani ametemewa matema.
Wengine wamemuuliza Mkemi kwamba hajui masuala yanayohusu uandishi wakati aliwahi kuwa mtangazaji kwamba Azam TV kazi yao ni kunasa matukio na kama walilinasa la Yondani kutema naye kutuhumu kutemewa, wanastahili lawama ipi?
Kauli hiyo ya Mkemi imekuja kuafuatia tukio la beki Yondani lililo gumzo hivi sasa mitandaoni kumtemea mate mchezaji, Asante Kwasi, katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi Jumapili.








Sasa ndio umekusudIa alikuwa na haki Yondani kumtemea mate Asante Kwasa bila ya sabsbu yoyote kwakuwa yeye alitemewa mate na jee una uhakika huyo Yondani katemewa mate bila ya sababu? Mkemi ni wazi kaumizwa kwakuwa timu yake imelazwa na kwakuwa hata mashabiki wa timu take walikuwa wachache mno kuwafanya wachezaji kukosa sapoti na huo ndio ukweli
ReplyDeleteHuyu Mkemi kichwa maji kweli kweli,kama kitendo hicho alichofanyiwa Yondani ktk match na Singida hakikutiliwa mkazo bado hakihalalishi kitendo alichokifanya Yondani dhidi ya Asante Kwasi, Mkemi acha ukichwa maji,CV na cheo chako havikuruhusu kutoa hija za hovyo hivi unajidhalilisha sana,tulia na tafuta njia nzuri.
ReplyDeletekosa halihalalishi kosa..............aweke na ile Ngoma akimpiga Ngumi Hassan Kessy
ReplyDelete..................Hata hivyo, Mkemi ameweka clip ya Azam TV inayoonyesha Yondani akiwa na mate eneo la sikio lake, akimtuhumu Batambuze kumtemea......ebho...........hii inaitwa negation of negation .............
ReplyDeleteHuyu Mkemi huwezi hata kidogo kumfananisha na Manara ambaye kwa hakika anajuwa kusema na mwingi wa hekima na busara ni furaha kwa kila analolisema na huku akiwa kipenzi kwa wengi
ReplyDeleteHoja ya kipuuzi kabisa. Kwa hiyo kwa kuwa alitemewa na yeye kutemea mtu ni halali? Kweli huyu akili zake haziko sawa. Wanasimba mpuuzeni kama alivyojipuuzisha
ReplyDelete