May 1, 2018



Polisi jijini LIverpool wametoa ulinzi maalum kwa kumpa askari wa kumsindikiza nyota wa kikosi cha Liverpool, Mohamed Salah.

Salah raia wa Misri, pamoja na ulinzi wa timu alilazimika kuongezewa askari mmoja ambaye alimsindikiza yeye wakati kikosi hicho kikiingia kwenye uwanja wa ndege jijini hapo.

Liverpool ilikuwa inaondoka kwenda Italia kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa jijini Roma, Italia  dhidi ya AS Roma, kesho.

Salah aliongezewa askari kutokana na kiu ya mashabiki kutaka kupiga naye picha, jambo ambalo lilisababisha hali hiyo.

Askari huyo alihakikisha Salah anaingia ndani katika eneo la uwanja wa ndege kabla ya kuungana askari wenzake na wenzake na kuondoka eneo hilo.









1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic