May 9, 2018


Baada ya kuwasili nchini jana kutokea Algeria kushiriki mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewaomba mabosi wake kutumia kikosi B.

Zahera amewaomba waajiri wake kutumia wachezaji wa kikosi cha vijana katika mechi za ligi zilizosalia ili kukipa nafasi cha kwanza kujiandaa na mechi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Mkongo huyo anaamini kuwatumia vijana hao kutatoa mwanya kwa kikosi cha kwanza kujipanga upya kwa ajili ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon utakaopigwa Uwanja wa Taifa Mei 16 2018.

Uamuzi wa Zahera kufanya hivyo umekuja kufuatia Yanga kuanza vibaya katika hatua ya makundi kwa kupoteza dhidi ya USM Alger ya huko Algeria.

Yanga itakuwa Uwanja wa Sokoine kesho kukipiga na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo leo inatarajia kusafiri kuelekea mkoani humo.


4 COMMENTS:

  1. Awana chakupoteza wa msikilize mwalimu ilitimu ifanye vizuri.ameangalia uwezo wa wachezaji hajaelewa inabidi apate mda wa kuisoma timu

    ReplyDelete
  2. Hamna viongozi wa kuelewa mantiki ya ombi lake.Watafikiria mapato bila ya kufikiria faida itakayopatikana kwa wachezaji kupata muda wa ziada wa kupumzika. BOK imeshapata bingwa waelekeze ngumi zao kwenye Conf.Cup .

    ReplyDelete
  3. Nimempenda sana huyu mwalimu anajua taaluma yake, ila kaja katika nchi ya kusadikika awawezi kumkubalia ombi lake.

    ReplyDelete
  4. Kuna maombi siyo maombi, wewe umepewa timu kama Mtaalamu halafu unaomba tena upangiwe Kikosi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic