May 4, 2018Na George Mganga

Uongozi Simba kupitia Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Salim Abdalla 'Try Again', umetangaza kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa dharura Mei 20 2018.

Simba wametangaza kufanyika kwa mkutano huo unalenga mabadiliko ya katiba kuhusiana na mfumo wa kisasa wa uendeshwa ndani ya klabu.

Tayari Simba wameshamtangaza mshindi wa zabuni aliyejitokeza kuwekeza hisa zake ambaye ni Mohammed Dewji, hivyo itakuwa ni mchakato wa mwisho kuelekea kukabidhiwa majukumu rasmi ndani ya Simba.

Mkutano hup unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo mitaa ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV