May 4, 2018Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, imetangaza kumsimamisha beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima, kwa kosa la kurudi Uwanjani kushangilia wakati akiwa amepewa kadi nyekundu.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 22 katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Bodi imetangaza kumsimamisha mchezaji huyo kuichezea Mbeya City mpaka pale shauri lake litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF kisha kutolewa maamuzi.

Mchezaji huyo alipewa kadi ya pili ya njano na nyekundu kufuatia kucheza madhambi dhidi ya mchezaji wa Yanga zikiwa zimesalia dakika chache mpira kumalizika.

Mchezo huo uliofanyika Mbeya, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

1 COMMENTS:

  1. Kupigwa kiwiko kwa mchezaji wa mbeyacity limeonekana ni kosa dogo ila mchezaji wa mbeyacity kuingia uwanjani na kushangilia goli akiwa tayari amepewa kadi limeonekana ndio kosa kubwa vipi kama mchezaji aliyepigwa kiwiko angefariki?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV