MWENYEKITI LIPULI ATOLEA UFAFANUZI SUALA LA KUWABANIA YANGA SALAMBA NA KUWAPA SIMBA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Lipuli umelitolea ufafanuzi suala linaloezwa kuwa iliwabania makusudi Yanga kuwaazimisha aliyekuwa mchezaji wao Adam Salamba na badala yake amesajiliwa Simba.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ramadhani Mahano, amezungumza na kueleza kuwa kuna vitu ambavyo Yanga waliwaeleza lakini walishindwa kwenda nao sawa.
Mahano amesema Yanga waliwapa taarifa kuwa mchezaji huyo asingeweza kutumika ndani ya timu tatu katika msimu mmoja kwani kanuni za soka haziruhusu.
Kiongozi huyo amefafanua akisema kuwa kwa mujibu wa TFF, CAF na FIFA hawaruhusu mchezaji mmoja kuzitumika klabu zaidi ya mbili ndani ya msimu mmoja hivyo ilikuwa ngumu kuwapatia.
Tayari mchezaji huyo ameshamwaga wino na wekundu wa Msimbazi ikiwa ni baada ya msimu kumalizika kwa kusaini mkataba wa miaka mwili na katika msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi hicho.
Yanga walitaka kumuazima na huenda baadae labda wauziwe kwa mkopo,lakini walionazo pesa wakamchota kirahisi na huku yanga ikingoja kuazimwa. Kweli inatia huruma. Iliyobaki sasa ni kuwaomba Simba wawaazime
ReplyDeleteHuyo asifanye watu watoto yanga wangemtumia ktk mashindano ya kimataifa sio kwenye ligi kahyo hyo dhana ya kutumika timu 3 haipo
ReplyDeleteTatizo nini? Kwani unapoomba lazima maombi yakubaliwe? Lipuli wala haina haja ya kujitetea kama suala ni wao kupata pesa, waliona kwenye kuazimwa mchezaji hakuna pesa, hivi unategemea wakubali tu kwavile ni Yanga?
ReplyDelete