May 30, 2018

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini, Ally Mtanda

Idara ya uhamiaji nchini imezitaka timu zote za mpira wa miguu zenye waajiriwa kutoka nje ya Tanzania kuomba vibali vya kufanyia kazi mapema.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili tu baada ya msimu wa ligi 2017/18 kumalizika huku dirisha la usajili likitarajiwa kufunguliwa siku kadhaa zijazo.

Kupitia Afisa Habari wa Idara hiyo, Ally Mtanda, amesema kuwa ni wakati mwafaka wa timu zote haswa zinazoshiriki Ligi Kuu Bara nchini kuomba vibali hivyo kwa makocha na wachezaji ili kuepuka kuleta usumbufu hapo baadaye.

Mtanda ameeleza kuwa hivi sasa ni wakati mwafaka wa viongozi wa timu hizo kutumia muda huu wa matayarisho kulifanyia kazi suala hilo kabla ya msimu mpya kuanza.

Mkuu huyo wa Idara ameamua kutoa taarifa mapema ili kuwakumbusha wahusika wa timu hizo ili baadaye kusije kukawa na malalamiko kuhusiana na kuchelewa kupatiwa vibali vya kazi kwa waajiriwa wao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic