Baada ya kuenea kwa tetesi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi kuhusishwa kuwa ameshamaliza na Simba, Yanga wameibuka na kutoa tamko.
Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa taarifa hizo hazina uhalisia wowote na anachokijua Tshishimbi alipowasilia Yanga alisani mkataba wa miaka miwili.
Ten ameeleza kuwa hana mengi zaidi ya kuzungumzia kuhusiana na Tshishimbi na badala yake amesisitiza akieleza kuwa Tshishimbi bado ni mchezaji wao.
Kiungo huyo mwenye asili ya Congo aliyewahi kuichezea Mbabane Swallows ya Swaziland alijiunga na Yanga Agosti 2017 na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Duh jamani Simba chonde chonde ..tunaomba poo
ReplyDeleteSimba hawana huruma!!. Jamani tuhutumieni. Mimi nilivosikia ni kuwa mchezaji ambae hsjalipwa kwa muda wa miezi mitatu mfululizo anayo haki ya kuvunja mkataba na wengine wanasema eti Simba ipo tayari kuwarejeshea yanga hela ya mwaka mmoja uliobakia na kwakuwa yanga wana shida ya hela wanaweza kukubali
ReplyDeleteNaamini wapo wachezaji wengi nje ya nchi ambao ni wazuri zaidi ya hawa akina SHISHIMBI hivyo ni vema Simba tuachane nao tuangalie kwingine kwani wenzetu watajenga hisia kuwa ni kuwakomoa. Japo walikua na kasumba ya kurubuni wachezaji wa SSC huko nyuma au yeyote alie ktk mazungumzo ya usajili na hata alieletwa toka nje kwa nia ya kusajiliwa. SSC tuachane na hiyo (Japo wao ilikua ndio zao huko nyuma) tutafute majembe mengine (kwa kuwa wapo ma star wengi wenye uwezo wa hali ya juu kuliko hawa)
ReplyDeleteNai subili huyo sapraiz maana mpira ni siasa kwahiyo hata sisi tulishituka kwa ajibu kuondoka kwahiyo tuvumiliane
ReplyDeleteUmenena. Wewe umesema machache lakini yameeleweka. Watuvumilie hii ni zamu ya Simba. Kwani Ajibu, Kessy, Yondani walichukuliwaje kwenda Yanga? Wasilaumu mtu wavumilie tuu
DeleteYanaga has a tradition of denying every thing and by the end of the day, the intended players disappear, surfacing elsewhere
ReplyDeleteGo Simba, go... Sajilini wachezaji wote waliopendekezwa na kocha bila kujali wanatoka timu gani. Tunataka kikosi cha ubingwa wa Afrika, kama tulivyotiwa hamasa na Rais Magufuli.
ReplyDeletesijui kama simba wanaangalia na kujifunza associated risks ya kusajili mapro, the risk is very high kama anayedhamini malio akajitoa na hili ndilo funzo huenda yanga wanalipitia sasa
ReplyDeleteHakuna Simba sajilini wachezaji wa kupambana kwenye kombe la Afrika, siyo vikinda kama akina Ajibu, Kessy, Juma Abdul tunataka mashine za kupambana na kuleta ubingwa kama akina Okwi, Kwasi, Bocco, Kapombe na wengineo. Tusirudi nyuma Tshishimbi, Chirwa, Pascal Wawa peleka Msimbazi tuuuuu.
ReplyDeleteProtas-Iringa
Huyo ndie mbadili wa Mo pamoja na Yondani. Anae kunyima kunde kakupunguzia??? Aondoke vije vifaa vya mana
ReplyDeleteMm siafiki simba kuchukua wachezaji wa yanga hata kama wa ndani sijaona wa kuchukuliwa pale,labda yanga ndio wasajiri kutoka simba.
ReplyDeletePOOO JAMANI POOO HUYU TSHITSHIMBI NDIO ROHO JAMANI POOO MKITAKA AJIBU WENU ARUDI SAWA TUONGEENI ILA THISHIMBI ABAKI
ReplyDelete