May 4, 2018



Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Simba, Mzee Hamis Kilomoni, ameibuka na kudai kuwa Simba haijafuata katiba baada ya kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura utakaofanyika Mei 20 2018.

Kilimoni ameeleza kuwa Simba imeenda kinyume na katiba kitu ambacho anakipinga huku akisema wanachama wake wamekuwa wakivutwa bila kujijua.

Mzee huyo ambaye ameonekana kupinga mchakato wa mabadiliko kwa muda mrefu, amezungumza kupitia Radio Efm akipinga Simba kuitisha mkutano huo.

Simba imetangaza kuitisha mkutano huo kwa ajili ya mabadiliko ya kikatiba huku ikielezwa ndiyo itakuwa safari ya mwisho ya kumkabidhi rasmi mzabuni wake, Mohammed Dewji Mo.

Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano uliopo mitaa ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

8 COMMENTS:

  1. Hatusumbui siku hizi. Njaa yake haiwezi kutibua mipango yetu. Bila mkutano watu watajaduliana vipi? Hawa wazee wanazeeka vibaya sana

    ReplyDelete
  2. Huyu kizee mwanga nini? Asitutake turejee katika swaum kama Ndala eh! Kikafie mbali kizee hiki

    ReplyDelete
  3. Huyu mzee Kilomoni vipi?...hawa ndio wachochezi wanaoleta vurugu kwenye vilabu.mkutano ulisharidhia kwa wanachama karibia 99% kupitisha mabadiliko ya katiba na hisa kupewa MO Dewji aliyeshinda zabuni.Huyu mzee anawashwa nini hasa?

    ReplyDelete
  4. Njaa mbaya sana! Miaka yote aliyokaa kama mdhamini kafanya nini!Ukipingana na mabadiliko yatakusomba tu ukafie mbele!!Babu pambana na hali yako!!!

    ReplyDelete
  5. Mzee mbona unatia aibu? Huenda ikawa yapo mambo akifaidika nayo na sasa hapo tena. na ndio katukwa na akili

    ReplyDelete
  6. Anaunyembelea uraisi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic