May 4, 2018



Na George Mganga

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, ameshindwa kujumuika na kikosi cha timu yake katika safari ya Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wameondoka jana kuelekea nchini humo wakiwa na jumla ya wachezaji 17 huku jina la Chirwa likikosekana katika orodha.


Mbali na Chirwa, kiungo wa kimataifa kutoka Congo, Papy Tshishimbi naye hajaungana na timu hiyo katika safari hiyo.

Kukosekana kwa wachezaji hao ambao ni mhimili wa kikosi cha Yanga kunaweza kukaathiri kwa namna moja ama nyingine sehemu ya kiungo na ushambuliaji kutokana na umuhimu wao kikosini.

Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, itapigwa Mei 6 2018, Jumapili ya wiki hii.

1 COMMENTS:

  1. HAPA KUNA KITU NYUMA YA PAZIA KUNA WADHAMINI WATATU WAKUBWA SASA KWANINI WANASHINDWA KULIPA MISHAHARA? WACHEZAJI MBONA HAWAPONI MAJERAHA? KWENYE MECHI MUHIMU KWANINI NDIPO UDHURU UNAIBUKA? WALE WENYE FEDHA WAKO WAPI YANGA? NIDHAMU YA WACHEZAJI MBONA IKO CHINI NANI ANAHUSIKA NA HILI? KIBALI CHA KOCHA KWANINI MCHAKATO UMECHUKUA MUDA? USHAURI YANGA IJITOE MASHINDANONI KULIKO KUTULETEA AIBU....HIVI TUKISIKIA WANAFUNGWA 8-0 KUNA KULAUMU? HII NI HATARI SANAAA....HIVI WAPENZI WA YANGA WENGI WANAUGUA NA KUFEDHEHEKA MWAKA HUU.....KWENYE MSAFARA VIONGOZI NI WENGI 11 NA TIMU ILIYOENDA NA YOSSO 17....MNAFANYA MASIHARA NYIE MNAENDA KUCHEZA NA MABINGWA WA ALGERIA WENYE MAANDALIZI NA MASHABIKI WENYE NGUVU....MBONA KILIO TUNAKITAFUTA WATANZANIA JAMANI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic