NDANDA WATOA KAULI HII BAADA YA USHINDI WA BAO 3-0 DHIDI YA MWADUI FC
Baada ya kuibuka na ushindi wa maba0 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa ligi uliopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona jana, uongozi wa kabu hiyo umesema bado una safari ngumu.
Kupitia Afisa Habari wa klabu, Idrisa Bandari, amesema kuwa kwa sasa wanahitaji kupigania alama tatu katika mchezo wao ujao dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga.
Bandari ameeleza kuwa wanapaswa kupambana ili kupata matokeo kwenye mechi ijayo na endapo watashinda watakuwa wamejiwekea asilimia 100 kuendelea kubaki kwenye ligi.
Ndanda itakuwa inawakaribisha Stand katika Uwanja wake wa nyumbani, Nangwanda Sijaona kuhitimisha safari ya michezo ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2017/18.
Ushindi wa jana dhidi ya Mwadui ulisaidia kuiweka kwenye mazingira mazuri ya kuendelea kusalia kwenye ligi, kilichobaki sasa ni kupata ushindi kwenye mchezo mmoja uliosalia.
0 COMMENTS:
Post a Comment