May 24, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mkuu wake wa Kitengo cha Habari, Dismas Ten, umesema kuwa unajiandaa kupigania alama tatu muhimu dhidi ua Ruvu Shooting.

Yanga itakuwa ina kibarua Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukipiga na Ruvu, mchezo utakaokuwa wa kukamilisha ratiba ya ligi msimu huu.

Kauli ya Ten imekuja kufuatia Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire kutamba kuwa wataifunga Yanga kwa jumla ya mabao 4-0 ili kuipa wakati mgumu wa kushikia nafasi ya pili.

Teni ameeleza kuwa maandalizi yanaenda vizuri kwa ajili ya kuwakabili Ruvu huku akisema lengo lao ni ushindi tu.

Yanga na Azam wanawania kumaliza nafasi ya pili baada ya kuukosa ubingwa na Yanga inahitaji kupata ushindi Ijumaa ili kujiwekea mazingira mazuri ya kushika nafasi hiyo.

Baada ya mchezo huo Yanga itakuwa tena Uwanja wa Taifa kukipiga na Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic