NENO LA MWAKYEMBE KUHUSIANA NA WALIOPINGA MABADILIKO SIMBA
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amefunguka kuhusiana na wachache ambao wamekuwa wakipinga mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu za Tanzania.
Hivi karibuni kumewakuwa na mapingamizi kadhaa kwa baadhi ya wanachama haswa wa klabu ya Simba ambayo ilianza mchakato wa mabadiliko kupinga ubadilishwaji wa katiba wa klabu hiyo.
Mwakyembe amefunguka na kuwashauri kuwa hakuna haja ya kwenda mahakamani na badala yake wanapaswa kufika Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kama wanadai haki zao za mpira.
Waziri huyo alisema hayo jana akiwa mgeni rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere, Dar es Salaam ambapo Simba walikuwa wanafanya mabadiliko ya Katiba kungia rasmi katika mfumo wa kisasa wa uendeshaji wa klabu.
Mwakyembe alieleza hayo kutokana na baadhi kutishia kuwa wataenda mahakamani kupinga mabadiliko hayo ya katiba huku wakieleza mkutano huo ulikuwa wa dharura.
0 COMMENTS:
Post a Comment