RAIS MAGUFULI KUWAKABIDHI SIMBA KOMBE UWANJA WA TAIFA, VIINGILIO VYATAJWA
Na George Mganga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 2018.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia, amesema kuwa wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo.
Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.
Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa maba0 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.
Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza majira ya saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.








This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMimi ni Simba lakini, siafiki wazo la kumuingiza Raisi kwenye siasa za usimba na uyanga. Na TFF isitumie kigezo cha ubingwa wa Serengeti Boys kutumika kuwapa kombe pamoja na timu ya Simba....Kwani Waziri wa Michezo hatoshi kuwa mgeni rasmi? TFF muwe makini sana msimuingize Raisi katika uhasama na watanzania walio wapenzi wa Yanga! Isije ikaonekana kuwa Uongozi wenu unamuhusisha Raisi kwenye upenzi na kuegemea upande mmoja wa timu fulani....athari zake ni kubwa hasa wakati huu akiwa madarakani....anaweza akahusishwa na kualikwa wakati hayuko madarakani....Waziri mwenye dhamana ya michezo angetosha tu kuwa mgeni rasmi
ReplyDeleteAsa hapo ndo umeandika nini?kila kitu ni kupinga tu huna hata hoja ya maana
DeleteMtazamo wake jamani msimlaumu handio walio sema ramadhani singano alpwi.bola aende akakuze kiwango chake nakupata maslai mazuri.naunaona mafanikio aliyonayo ramadhani singano jinsi kiwango kilivyo kua panga pangua yumo kikosini na amekua gumzo nnchini kwa sasa.
ReplyDeleteWe we kinakuumanini ulitakstukualike wewe wacharoho ya kwanini uweniyanga amasimba
ReplyDelete