Mshambuliaji wa klabu ya Liverpoolna timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa mwaka nchini England kupitia tuzo ambayo hutolewa na Waandishi wa Habari za Michezo.
Salah ameshinda tuzo hiyo leo inayojulikana kama Football Writers Association (FWA) kutoka kwa waandishi wa soka nchini humo.
Tuzo hiyo imekuwa ya kwanza kwa mchezaji wa Kiafrika kuitwaa tangu kuanzishwa kwake.
Nyota huyo ametwaa tuzo hiyo akiwa anatarajiwa katika kikosi kitakachoanza dhidi ya AS Roma kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho Jumatano.








0 COMMENTS:
Post a Comment