May 14, 2018



Baada ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Dodoma Combine kumalizika Uwanja wa Jamhuri kwa sare mabao 2-2, mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18 Simba SC, jana walifanyiwa hafla ya mlo wa jioni na wabunge wanaoishabikia timu hiyo.

Kikosi hicho kilifanyiwa hafla fupi na wabunge ambao wanaishabikia Simba kwa kujumuika nao katika chakula cha jioni jijini Dodoma.

Simba ipo Dodoma baada ya kuwasili jana ikitokea mjini Singida kushiriki mchezo wa ligi ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United.

Baada ya kuwasili jijini humo jana na kujumuika katika mlo wa jioni na wabunge, kikosi hicho kimepata mwaliko wa kwenda bungeni leo kupata pongezi baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa ligi.

Simba watapata wasaa wa kuhudhuria kikao cha leo katika Bunge la Jamhuri ili kupata pongezi zao baada ya kuchukua ubingwa huo wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Simba watakuwa wanaweka rekodi ya kufika Bungeni ikiwa ni mara ya kwanza tangu Dodoma ipewe hadhi ya kuwa jiji.

2 COMMENTS:

  1. Inafurahisha mwaka huu na ijayo. Ahsante milionea Mo. Mungu akubariki na utakumbukwa daima ndani na nje ya Tanzania yetu. Hayo ni mafanikio ya kwanza tu na tutashuhudia mengi usoni chini ya ukarimu wake ambae hakuwa na uchu wa kuwa kiongozi bali mapenzi yake kwa timu

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Simba kwa ubingwa ila SIMBA na watanzania tuanze kujipanga kuanzia sasa na maandalizi ya mashindano ya kimataifa. Kwa simba tunatakiwa kuanzia tulipoishia kwa Almasry. Tunatakiwa kujiuliza na kujifunza kwanini tulishindwa kuvuka kigingi cha Almasry. Wachezaji na benchi lao la ufundi walijitahidi sana ila ushahidi uliowazi SIMBA walihitaji ziada ya wachezaji wenye uzowefu katika mashindano ya kimataifa wenye hasa wale jitihada binafsi kwenye nafasi za ulinzi na ushambuliaji. Vile vile timu inahitaji mechi za majaribio za kutosha na timu zenye uwezo zaidi barani Africa au hata nje ya la bara Africa sio kitu rahisi lakini ndio hali halisi. Kwa hivyo kikao cha wabunge cha ukaribisho cha kuipongeza SIMBA kitumike kuwa kikao cha mkakati kwa ajili ya maandalizi ya ushirki wa SIMBA katika mashindano ya kimataifa. Kuna wachezaji kadhaa wa kunzia wa hapa hapa nyumbani SIMBA inapaswa kuondosha muhali na kuanza mikakati ya kuwasaini ili kukijazia nyama kikosi kilichopo sasa pasi ya mawazo ya kocha anashauri vipi lakini kitu kizuri na bora huwa hakijifichi, wachezaji kama Obrian Chirwa wa Yanga.Ni mchezaji mzuri SIMBA inapaswa kupigania saini yake kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kimataifa. Kinachomsumbua Chirwa ni hali isioeleweka ya maslahi yake pale yanga kitu ambacho kinaonekana kumuathiri kisaikolojia vile vile hata kwenda zake kuamua kulima mahindi. Lakini kama Chirwa atatua SIMBA na hali ilivyo hivi sasa basi anaweza kuwa mchezaji atakaeleta mapinduzi makubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba ni mchezaji mwenye nguvu kaliba ya Aristide Banzi wa Almasry. Mchezaji mwengine SIMBA wa kutafutana lawama ni Shafii Batambuze wa Singida United hata kama Singida nao wao wapo katika harakati za kushiriki mashindano ya kimataifa lakini sio sababu ya SIMBA ya kutoweza kwenda kufanya mazungumzo ya kuingia mkataba na wachezeji kama Simba wataona anawafaa na sheria inaruhusu. Muheshimiwa Mo itabidi awe na ustamilivu na timu yake ya nyumbani kuchukiwa wachezaji.
    Licha ya number anayocheza Batambuze kuwa na upinzani mkali pale Simba lakini Batambuze ni mchezaji wa level ya juu katika kanda yetu hii ya Africa mashariki hata na kati ya Bara letu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic