May 14, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Azam kupitia kwa Afisa Habari wake, Jaffer Idd Maganga, umesema kuwa baada ya kuona ubingwa ni ndoto kwao, sasa umejipanga kumaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya timu hiyo kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Stand United kwa kufungwa mabao 2-1 huko Shinyanga.

Azam ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hivi sasa wakiwa na pointi 52, wanaiombea Yanga isifanye vizuri ili waweze kusalia kwenye nafasi hiyo kujiwekea heshima.

Azam watakuwa wanapambania kushika namba mbili kwenye msimamo ambayo ilikaliwa na Yanga kwa muda mrefu wakati ligi ikianza.

Jana Yanga iliendelea kufanya vibaya baada ya kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika mechi ijayo, Azam watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex wakiirabisha Majimaji FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic