May 12, 2018



Wakati Simba wakijiandaa kuapizwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara watakapotua uwanjani leo Jumamosi kuwavaa Singida United, wapinzani wao hao wamesema kuwa hawatawapigia makofi ya heshima.

Timu hizo zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida katika mechi hiyo ya ligi ambayo Simba wataingia uwanjani wakiwa tayari mabingwa baada ya wapinzani wao Yanga kufungwa mabao 2-0 na Prisons mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Tukio la aina hiyo la kugoma kuwapigia makofi wapinzani wao waliwahi kulifanya Real Madrid hivi karibuni walipopambana na Barcelona ambao tayari walikuwa mabingwa katika mechi ya El Classico ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Meneja Mkuu wa Singida, Ibrahim Mohamed alisema kuwa wapinzani wasitarajie kukutana na tukio hilo la kupigiwa makofi katika mechi hiyo. Ibrahim alisema, wapinzani wao kitu watakachokipata ni kupongezwa tena kama wakifungwa lakini siyo kupanga mstari na wachezaji wa Simba kupita katikati na kuwapigia makofi.

“Hakuna sheria inayosema kuwa wapinzani wakiwa mabingwa siku ya mchezo wapinzani wao wakapange mstari na wao mabingwa wapite katikati na kuwapigia makofi.

“Hivyo, kwetu hakuna kitu kama hicho tena nirudie hakuna, sisi tutaingia uwanjani kwa lengo moja la kupata ushindi na siyo kitu kingine, hivyo katika mechi tunataka ushindi kwa lengo la kulipa kisasi. “Simba wao kama wanataka kupigiwa makofi, basi wasubirie mechi nyingine zitakazofuata watakazozicheza wakapigiwe makofi lakini siyo kwetu,” alisema Ibrahim.

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Kwani Simba kutangazwa bingwa kwako kunauma nini kiongozi? Je usipopiga makofi ndo ubingwa hauendi Msimbazi, acha maneno ya kupotosha watu kama hutaki kupiga makofi sawa, kwani umeambiwa lazima upige makofi?

    ReplyDelete
  2. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Eti hatutopiga makofi tunataka lipa kisasi 😎😎😎😎 nimeona.

    ReplyDelete
  3. Katia aibu sana namna alivyokua hana ufahamu wa soka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic