May 12, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza rasmi kutuma barua kwa uongozi wa Lipuli ukiomba kuwapatia mchezaji Adam Salamba ili kuja kikiboresha kikosi cha kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ilithibitisha jana kutuma barua hiyo ikiwa na matumaini ya kumpata mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu msimu huu wa ligi uanze.

Salamba ambaye ni mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Machi, ameingia kwenye rada za Yanga ikiwa inajiandaa na mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa sambamba na ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.


Mei 16 2018 Yanga itakuwa inawakaribisha Rayon katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa pili katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ikiwa ni baada ya kupoteza ule wa kwanza kwa idadi ya mabao 4-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Ujio wa Salamba unaweza ukaimarisha safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi hicho haswa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na pengine kuwa mbadala wa Donald Ngoma ambaye ana majeraha ya muda mrefu.

3 COMMENTS:

  1. Yanga inataka kufanya biashara gani ya kijinga ya kutaka kuwamaliza hawa vijana? Yanaga isitake kutumia kisingizio cha mashindano ya kimataifa kuwahadaa hawa watoto waingie mikataba ya kijinga baadae ikaja kuwa matatizo. Kwa kiasi fulani Yanga inataka kuwatumia hawa watoto sio kuwasidia. Unamumbuka Samata alipogoma kuichezea SIMBA kwa sababu ya kutotimiziwa ahadi zake? Samata hakufanya vile kwa kuwa alihitaji sana gari alikuwa anajua gari atakuja kulipata huko endako ila alionyesha jinsi gani alivyokuwa anjitambua na kutokubali kutumika kwa motisha hewa. Hawa akina Salamba sio wachezaji wa mkopo kwa klabu kama yanga. Ni wachezaji wakuuzika hata nje ya nchi au mkopo kwa klabu zenye nafasi zaidi za wao kujiendeleza huko nje ya nchi. Watanzania tumelala sana ni watu waoga wa kujaribu na ndio maana hamuna mawakala wa uhakika tunasubiri mpaka vilabu vya nje viwaone vijana wetu wenye vipaji badala ya sisi kuwalazimisha kuwaona. Na kwa hali hii watanzania tutasubiri sana. Wahenga walisema biashsra itangwazayo ndio itokayo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hapa kaka naona unaleta usimba na uyanga. haya mashindano pia ni fursa kwa kijana huyu kuonekana. unataka afanye nini zaidi ili aonekane?

      Delete
    2. Amelewa huyo. Je salamba anauwekano wa kujiuza kimataifa akiwa lipuli au yanga? Pia vijana hawapotezwi na timu bali wanabweteka wao mfano busungu, mateo antony, mahadhi nk. Wanapewa mafasi hawazitaki, kwann timu isilete wengine. Kina samata banda msuva nizar nk walionekana kupitia mashindano makubwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic