May 25, 2018




Klabu ya Al Hilal ya Sudan imeingia mkataba na mchezaji, Mtanzania, Thomas Ulimwengu, kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu.

Al Hilal imemsajili Ulimwengu kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili tayari kuanza kukipiga ndani ya Waarabu hao.

Timu hiyo imeshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi nchini humo ikiwa imejikusanyia pointi 33 katika michezo 13 iliyocheza.

Ulimwengu amejiunga na Al Hilal baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza soka tangu aachane na timu ya AFC Eskilstuna ya Sweden aliyokuwa akiitumikia.

Winga huyo pia aliwahi kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Congo sambamba na Mshambuliaji Mtanzania mwenzake anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji hivi sasa, Mbwana Samatta.

Mara ya mwisho, Ulimwengu alisajiliwa na klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden  akitokea kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo ambayo kabla ndiyo iliyomuuza kwenda Mazembe lakini akashindwa kuonyesha cheche kutokana na kuandamwa na maumivu ya goti.

5 COMMENTS:

  1. TOKA NIJUE HII BLOG IMEKUWA YA MIPASHO NA UONGO ULIOKITHIRI SASA HIVI KILA TAARIFA NINAYOONA MMEANDIKA NAIFATILIA KWA UHAKIKA SEHEMU NYINGINE MAANA HAMKAWII KUTUDANGANYA NYIE, KAMA HAPO MMEANDIKA ETI ALHILAL AMECHEZA MICHEZO 33 NA ANAPOINT 33,WAKATI AL HILAL AMECHEZA MICHEZO 13...AMESHINDA michezo 10 amedraw mi3, KWA UONGO TU HII BLOG SHIKAMOO, alaf mbaya sasa hii sio mara ya kwanza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma makala vizuri, huenda macho yako ndio hayaoni vizuri. Nanukuu kama mwandishi alivyoandika, "Timu hiyo imeshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi nchini humo ikiwa imejikusanyia pointi 33 katika michezo 13 iliyocheza." Wapi ameandika michezo 33?

      Delete
  2. Mbona ndugu unakwenda kwenye kuahukumu, kukosea ni jambo la kawaida kwa mwandishi badala ya kuweka michezo 10 akaweka michezo 33, hata kama kiuhalisia haiendi sawa. Ila ujumbe mkubwa hapo ni kwa Thomasi Ulimwengu kuhamia Al Hilal na wala siyo idadi ya points na michezo ya timu hiyo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Ni sawa ndugu Elisha Issaya badala ya kuandika 13 akandika 33 kama typing error kiongozi.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. Watu Wamekaa Kuwakosoa Wengine kama Wao Wapo Sahihi Kila Wanachofanya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic