May 25, 2018

COASTAL UNION WAKATI IKIWA LIGI KUU BARA


Huku wakielekea kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao baada ya kupanda ligi kuu uongozi wa Coastal Union umefunguka  kwa sasa unashindwa kuweka mipango yake sababu ipo kwenye mchakato wa  kusaka wadhamini kwanza.
 Coastal ni moja kati ya timu sita zilizofanikiwa kupanda ligi kuu msimu huu na sasa ipo kwenye mchakato wa kusaka wadhamini kabla ya kuanza usajili wao.

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Mguto, alisema kuwa mambo mengi wanashindwa kufanya kwa sasa mpaka wakipata wadhamini ndipo wataanza kuweka mipango yao.

“Timu kwa sasa ipo bize kusaka udhamini kwanza ndiyo mambo yaweze kwenda, bila hivyo itatusumbua huko mbele tumeamua kufanya hivyo ndiyo maana tunashindwa kusema kuwa timu inaanza lini mazoezi mpaka tuweze kulikamilisha hilo.

“Baada ya kumaliza hilo la udhamini ndiyo mipango yetu yote tunaweza kuianika na lengo letu ni kuanza maandalizi mapema ilikuweza kujipanga vyema kukabiliana na ligi msimu ujao,” alisema Mguto.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic