May 7, 2018




Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kimeanza vibaya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya makundi kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa USM Alger katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Julai 5 1962.

Yanga iliyokuwa inawakosa nyota wake muhimu katika mchezo huo imekumbana na kichapo hicho kikali ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua hiyo.

Mabao ya USM Alger yametiwa kimiani na Oussama Darfalou katika dakika ya 4 ya mchezo, bao la pili likifungwa na Farouk Chafai dakika ya 33. Mpaka mapumziko Yanga walikuwa nyuma kwa mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili kilipoanza kilizidi kung'ara kwa wapinzani ambapo mnamo dakika ya 54 Mezziane alitikisa nyavu za Yanga na kuongeza bao la tatu.

Na zikiwa zimeongezwa dakika 4 mchezo kumalizika, Yanga ilifungwa tena bao la 4 na la mwisho na mchezaji Mohamed kwa njia ya penati, na kufanya matokeo hayo kwa ujumla yamalizike kwa wenyeji kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao 4-0.

3 COMMENTS:

  1. Duuuuuuh ......bahati mbaya tu.

    ReplyDelete
  2. Kutangulia sikufika tuna wasubiri huku tushawajua wanavyo cheza tukiwana namajembe yetu ngoma,tambwe magoli,ibrahim ajibu kijana machachari alieshushushwa na mungu hawatoki,huku kuna chilwa.nakipa tunawawekea kabwili natumai kanavaro yondani watakua vizuri.kama kawaida yanga inaanzaga vibaya mwisho inamaliza vizuri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic