May 20, 2018


Na George Mganga

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amebariki mabadiliko ya katiba Simba ambayo yanaenda kuupokea rasmi mfumo mpya na wa kisasa wa uendeshwaji wa klabu hiyo.

Mwakyembe ameeleza hayo punde kwenye Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam ambapo Simba wanaendelea na Mkutano Mkuu wa dharura kwa ajili ya maboresho ya katiba yao.

Waziri huyo amesema ni wakati mwafaka sasa kwa klabu za Tanzania kuingia katika mfumo huu ambao umejikita kibiashara na wenye mafanikio makubwa huku akieleza kuwa haukwepeki.

Aidha Mwakyembe amempongeza Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'Mo' kwa kuamua kuwekeza ndani ya Simba akiamini ataibadilisha zaidi klabu hiyo kuweza kufika mbali kimataifa.

Baada ya kueleza hayo, Mwakyembe amesema serikali imeruhusu rasmi mabadiliko hayo kwa kuzingatia Mwekezaji lazima awekeze kwa asilimia 49 na wanachama wasalie na 51.

2 COMMENTS:

  1. Asante waziri mwakyembe pia nichelee kumshukuru Mo wanasimba tunataka mpira uchezwe na sio mambo ya kwenda Fifa na kutuletea wachezaji miradi ya watu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic