April 17, 2020



HABARI kubwa kwa sasa ni suala la mchezaji wa Simba, Clatous Chama kuwindwa na watani wa jadi wa muda wote ndani ya ardhi ya Bongo ambao ni Yanga.

Mambo yamekuwa mengi ila muda unazidi kukatika taratibu kutokana na habari kuwa nyingi katika hili ila lazima ukweli uwekwe bayana na kila kitu kiwe wazi katika hili.

Mtazame ambaye ananukuliwa kwamba ndiye amesema kuwa amefanya mazungumzo na mchezaji Chama ambaye ni kiongozi mkubwa ndani ya Yanga.

Fredrick Mwakalebela yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga ni kiongozi makini ambaye anajua weledi wa kazi za masuala ya mpira pamoja na ishu zote za usajili.

Nafasi ya kuwa kiongozi ndani ya Shirikisho la Soka kwa muda mrefu inambeba na kumfanya awe na uzoefu katika masuala ya usajili achilia mbali kanuni na utaratibu wa kuzungumza.

Ni ngumu kuamini kwamba hajui anachokifanya ila ameweka wazi nia yake ilikuwa ni utani na ameomba msamaha kwa kuwa Uongozi wa Simba ulianza kuchukua hatua kwa uzito.

Kikubwa ambacho kinapaswa kiwekwe wazi hapa ni namna ya uwazi kwa wachezaji na mkataba wao unavyokuwa ili kuepusha hizi sarakasi.

Timu kubwa zimekuwa na kawaida ya kuficha mambo ila pale inapotokea tatizo ndipo kila mmoja anapotaka kutafuta pa kutokea ili amkomoe mmoja ama kuonesha kwamba yeye ni mwamba katika jambo fulani analofanya.

Wakati ule wa Papy Tshishimbi tumeona kwamba uongozi wa Yanga ulitumia busara kwa kukaa mezani na mchezaji na kuzungumza naye ila kwa sasa upande wa pili ishu ya Chama imekuwa kubwa na imegonga hodi ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Haina maana kwamba nawakataza Simba kufanya hivi hapana ila ukweli wa mkataba wa Chama upoje, ni mwaka mmoja kweli ama miezi sita imebaki hivyo kutokana na presha basi viongozi mnataka kuonyesha kwamba mpo makini katika hili kumbe ni danganya toto?

Twende katika hili tujikumbushe wakati ule kabla ya baadhi ya wachezaji kuondoka ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima twende na James Kotei hawa nyota wakati ule ilikuwa ukiwauliza wao walikuwa wanasema bado wana mkataba ndani ya Simba.

Mwisho wa siku kila mmoja alisepa zake na waliondoka bure kabisa kwa kuwa hawakuwa na mikataba ndani ya Simba na sasa wapo sehemu nyingine maisha yanaendelea hivyo katika hili la Chama linafikirisha na ni somo kuhusu uwazi wetu.

 Pia tayari Mwakalebela ameomba msamaha kwa ajili ya suala hili nalo lisipuuzwe kwa kuwa aliamini ni utani, kwa sasa ni lazima iwe fundisho kwa wengine na kutazama mipaka ya utani.

10 COMMENTS:

  1. Kwa kweli hujaeleweka ulicho andika..inshu mkataba wa Chama ama kuongelea mchezaji mwny mkataba?na kama hana huo mkataba kwa nini aombe msamaha?

    ReplyDelete
  2. We mwandishi wenzako wanakufanya. Papy Tshimbi alibakisha mkataba wa miezi sita ndani ya yanga hivyo hata kama simba waliamua kufanya nae mazungumzo ilikuwa haki yao kabisa. Kama ulivyokwishakusema kuwa Mwakalibela ni mtu makiini na mzoefu katika masuala ya michezo hivyo inazihirisha zaidi kuwa alikuwa anajua nini alichokuwa akikifanya kumchokonoa mchezaji ambae yumo ndani ya kandarasi ya muda mrefu.Ni mawazo pumba na yasiyo na mshiko hata kidogo kuilaumu simba kutoweka hadharani mikataba ya wachezaji wake kwa mtu kama mwakalibela ambae alishahudumu kwenye nafasi nyeti ndani shirika la mpira nnchini. Labda kwa kutumia jina lake na umaarufu wake ndani ya TTF ndio mwakalibela kunapompa kiburi cha kutoheshimu kanuni za soka nchini.Na hapana shaka uweledi wa mwakalibela katika masuala ya uendeshaji wa mpira nchini ndio uliopelekea uongozi wa simba kulichukulia suala hili la chama serious na ni vyema kuwapongeza simba kwa msimamo wao imara juu ya suala hili ili kukomesha mambo ya hovyo kutoka kwa viongozi wetu ndani ya soka letu.

    ReplyDelete
  3. Kama hana mwaka 1 au pungufu itajulikana tff sio kwako mwandishi. Busara unataka utumike vipi sasa? Tshishimbi wapi simba watangaza kupitia viongozi wao kuwa wanataka kumsajili? Acha wajifunze kwa adhabu. Hakuna namna, kama mwakalebela alikuwa anajua kama uvyodai kwann aombe msamaha? Acha ukanjanja.

    ReplyDelete
  4. Kumbe na nyie waandishi huwa hamtunzi kumbukumbu? Inatua wasiwasi ktk weredi wenu ktk kaz zenu.
    Nikukumbushe tu kidogo, unakumbuka wakati Simba wanatamburisha wachezaji waliowapa mikataba mipya na na kuwaongezea kandaras wachezaji waliokuwa nao kikosini kupitia kurasa zao za Instagram na YouTube,,
    Je, Ww mwandishi hukuiona sura ya Chama, pamoja na kandarasi iliyojifafanua zaidi kuhusu kuongezea muda wa kuendelea kuitumikia Simba ilihali alikuwa hajamaliza muda wake wa awali wa miaka miwili?
    Ushauri wangu kwenu Waandishi;
    Kuwenu na kumbukumbu kwa Ajili ya marejeo ya matukio ili kupunguza sintofahamu ktk kuandika makala zenu zinazohusu wachezaji..

    ReplyDelete
  5. Hivi kweli Mwakalebela alishindwa kuulizia TFF mkataba wa Chama?TFF si ndio wana-register wachezaji kucheza ligi na nina vyoelewa ya kuwa mchezaji bila kuwa na mkataba na klabu hawata mruhusu kucheza ligi.Na isitoshe alishindwa nini kwenda kupata ukweli wa mkataba toka Kwa meneja wake Chama na akaamua kusema amezungumza na mchezaji? Baadaye anakuja mbele ya kamdanasi kuomba samahani kuwa ulikuwa utani.Je anajua embarrassment aliyompa mchezaji?Mchezaji si anaonekana sio muanifu Kwa klabu yake
    inayoendelea kumlipa mshahara ndani ya mkataba.Mwandishi bila soni unakuja mbio-mbio kutuletea hoja zako pumba na ambazo hazina mashiko.Jitafakari ndugu mwandishi kuwa Sheria zimewekwa ili kuepusha migogoro.

    ReplyDelete
  6. Kila mtu ajitanie mwenyewe kuanzia sasa...tukisikia fyokofyoko tunaanza na wewe

    ReplyDelete
  7. Hivi wewe kanjanja ndio unajua kuliko Simba muda wa mkataba wa Chama?Hivi Simba wana kichaa kuwaripoti Yanga kuhusu mkataba wa Chama huku wakijua kwamba umemaliza miezi 6?
    Weledi au hata common sense inatosha kukujuza kwamba Mwakalebela amefanya kosa. Wewe kanjanja unajaribu ku balance stori kwa kujaribu kuficha kosa la Mwakalebela ama kwa upenzi au kwa kukosa weledi.

    ReplyDelete
  8. Makala nzuri, hongera Saleh Jembe

    ReplyDelete
  9. Makala nzuri kwa vile inaonesha ni jinsi gani mwandishi alivyo msahaulifu na asiyejali kurejea matukio kujua kwa uhakika anachokishabikia. Au ndiyo u-Yanga umemhusu?

    ReplyDelete
  10. Makala ya hovyo. Mwandishi ukiwa muongo usiwe msahaulifu.Hauna kumbukumbu au unafanya makusudi kwa sababu ya upenzi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic