May 26, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kujipanga na mechi ya kuhitimisha safari ya mechi za ligi dhidi ya Azam FC itakayopigwa Jumatatu ya wiki kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten, amesema baada ya sare dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa jana, sasa wanaanza maandalizi ya kuweka heshima dhidi ya Azam kuhakikisha wanashinda.

Ten amesema kinachofuata sasa hivi ni kuhakikisha wanapata matokeo watakapokutana na Azam walau waweze kumaliza ligi wakiwa namba mbili kwenye msimamo wa ligi.

Matokeo ya 2-2 dhidi ya Ruvu jana yanawalazimu Yanga kushinda dhidi ya Azam ili waweze kushika nafasi ya pili, na endapo mechi itamalizika kwa droo, hawatoweza kuwapiku Azam kwenye nafasi hiyo.

Yanga mpaka sasa ina alama 52 wakati wapinzani wao Azam wamejikusanyia pointi 55, hivyo mechi itakayowakutanisha Jumatatu kama Yanga atashinda ataishusha Azam na kupanda juu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic