May 3, 2018





Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wake Yanga mwishoni mwa wiki.

Furaha hiyo ilimfanya msemaji wao kuingia uwanjani kumalizia shangwe na mashabiki wao.

Lakini Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei Mosi, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.


Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

2 COMMENTS:

  1. Jambo dogo hilo wamekutana kulijadili mambo makubwa wanafunika kombe mwanaharamu apite Tff ina watu bwana tofauti na mashirikisho mengine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic