May 12, 2018



Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka kwa kueleza kuwa atawapigia simu bodi ya ligi ya TFF ili wamruhusu ashangilie leo.

Manara amesema hayo kufuatia kupewa onyo la kungia Uwanjani na kuanza kushangilia baada ya mchezo uliopita dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga uliofanyika Uwanja wa Taifa Aprili 29 2018.

Mkuu huyo wa Idara ya Habari Simba, ameeleza atafanya hivyo ili furaha yake isipotee kwa maana itakuwa ngumu kujizuia endapo Simba itapata matokeo dhidi ya Singida United.

Simba itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida kukipiga na walima alizeti hao walio na kumbukumbu ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya awali kwenye mzunguko wa kwanza.

2 COMMENTS:

  1. huyo hafai kuwa kiongozi wa soka hata siku moja hayuko serious kabisa abaki na ushabiki tu

    ReplyDelete
  2. Hujaona Jörgen Klipp akishangilia? Conte je?Mourinho akifanya sliding na suti baada ya kushinda? NI kosa kuonyesha mapenzi kwa timu unayoiongoza? Sababu yako ya kusema hafai luwa kiongozi ni ipi?Mtu umefanikiwa kuwahamasisha wanachama na wapenzi 40000 kuingia kwenye na kushangilia kwenye mechi dhidi ya Yanga ni kiongozi mzuri.Ubingwa wa Simba msimu huu amechangia sana.Wanasimba tunajua mchango wake na hatubabaishwi na protokoll za wavaa suti.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic