June 14, 2018


Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania anayekipiga katika klabu ya Baroka iliyopo Afrika Kusini, Abdi Banda, yupo mjini Zanzibar kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Banda amesafiri kuelekea mjini humo akiwa na mchumba wake, Zabibu Kiba ambaye ni mdogo wake na nyota wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Alikiba, ikiwa ni sehemu ya kumaliza likizo yake baada ya Ligi Kuu Afrika Kusini kumalizika.

Banda amefuata nyayo za nyota wa Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama, ambaye alikuwa mjini humo siku chache zilizopita  kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Imekuwa ni kawaida kwa wachezaji wengi haswa wa kimataifa kwenda Zanzibar pindi msimu wa ligi zao unapomalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic