June 14, 2018


Mwenyekiti Mkuu wa Kamati ya Maalum ya kuivusha Yanga wakati huu wa mpito, Abassi Tarimba, amefunguka na kusema anaunga mkono kitendo cha viongozi wa klabu hiyo kufanya uamuzi wa kujitoa kwenye mashindano ya KAGAME.

Tarimba amesema isingewezekana kwa Yanga kushiriki kutokana na namna ratiba hiyo ilivyokuwa ikiwa ni wiki mbili kabla, jambo ambalo lilikuwa gumu kwao.

Aidha, Tarimba amesema wachezaji wengi wa Yanga hawana mikataba hivyo ingekuwa vigumu kuweza kucheza mashindano hayo yanayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Yanga walituma barua TFF ya kujiondoa kwenye mashindano hayo wakieleza kuwa wamewapa wachezaji wao mapumziko kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Julai 18 watakuwa wanacheza ugenini na Gor Mahia FC ya Kenya.


1 COMMENTS:

  1. Hakuna cheo duniani kote cha MWENYEKITI MKUU mwandishi hii ni mara ya pili wiki hii unalirudia meno hili unakosea. Mwenyekiti ni Mwenyekiti. Katibu ndio tunakuwa na Katibu Mkuu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic