BREAKING: LOPETEGUI AFUKUZWA KAZI KUINOA TIMU YA TAIFA YA SPAIN BAADA YA KUJIUNGA MADRID
Julen Lopetegui amefukuzwa kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Spain ikiwa ni siku moja atangazwe kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Real Madrid.
Lopetegui amefukuzwa kazi ili kuepuka kuleta mkanganyiko ndani ya kikosi cha timu ya taifa hilo ambayo ipo nchini Urusi kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia.
Rais wa Shirikisho la Soka Spain, Luis Rubiels mapema leo aliitisha kikao na viongozi wenzake wa shirikisho hilo kujua mustakabali wa Lopetegui baada ya kutangazwa na Madrid kuchukua mikoba ya Zinedine Zidane.
Taarifa zilieleza kuwa Lopetegui angeweza kuleta mkanganyiko kwa timu ya taifa ya Spain ya kushindwa kuwapa nafasi wachezaji wa FC. Barcelona na Atletico de Madrid ambao wapo kikosini kwa sababu ya upinzani baina ya klabu hizo na Real Madrid.
Bodi ya Shirikisho hilo Spain pamoja na Rais wameazimia kumfukuza kocha huyo kibarua hicho na badala yake atatangazwa mwingine kurithi nafasi yake ili kukiongoza kikosi kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.
0 COMMENTS:
Post a Comment