Mudhathir Yahaya ameamua kurejea Azam FC akimfuata kocha wake, Hansa van der Pluijm.
Mudathir amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC.
Pluijm amejiunga na Azam FC akitokea Singida United.
Kabla Mudathir na Pluijm walikuwa pamoja na kocha huyo alimteua kiungo huyo kuwa nahodha wake.
Navyojua ni kuwa dirisha la usajili kwa ajili ya msimu ujao litafunguliwa tarehe 15, lakini kinachonishangaza ni kuwa kama timu mbili au tatu (Azam, Singida united, na simba) zinawapa mikataba wachezaji kabla ya muda uliowekwa kikanuni....sasa sielewi sababu ni zipi....lakini linaweza kuchangia kuwepo na mapingamizi mengi katika kupitisha usajili wa hawa wachezaji kwa msimu ujao. Mchezaji anaweza kufanya mazungumzo lakini hatakiwi kupewa mkataba kabla ya muda wa usajili kufunguliwa. Hata kama mchezaji husika amemaliza mkataba na klabu yake, bado haruhusiwi kikanuni na kisheria kusaini mkataba nje ya muda wa usajili.....Naomba ufafanuzi wa kisheria na kikanuni lakini sio matusi!
ReplyDelete