SHADRACK NSAJIGWA ATHIBITISHA RASMI KUACHIA NGAZI YANGA
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ameachia rasmi ngazi katika klabu yake baada ya mkataba wake kumalizika.
Nsajigwa aliingia katika benchi la ufundi la klabu hiyo wakati George Lwandamina akiwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho kabla ya ujio wa Mkongomani, Mwinyi Zahera.
Nsajigwa anaondoka Yanga ikiwa ni siku moja tu baada ya kuondolewa katika mashindano ya SportPesa Super Cup inayoendelea mjini Nakuru, huko Kenya.
Yanga iliondoshwa na Kakamega HomeBoys kwa mabao 3-1 Jumapili ya June 3 2018 uliopigwa kwenye Uwanja wa Afraha Stadium.
Kuondoka kwa Nsajigwa kutakuwa kunamfanya kocha Noel Mwandila kusalia kwenye benchi la ufundi la Yanga kama Msaidizi pekee.
Maskini Yeboyebo! Sasa timu munamuachia nani au Mzee Akilimali!
ReplyDeleteAtakuja kukumbukwa Nsajigwa. Mtu aliyeichezea timu hiyo kwa miaka mingi na baadae kuwa Kocha Msaidizi ana uchungu na timu.
ReplyDeleteKutokana na maamuzi ambayo kwa hivi sasa timu ya Yanga inafanya itakuja juta baadaye. Wajue matatizo yameumbwa yapo wanapaswa kukaa chini na kuangalia njia ya kutokea badala ya kushutumiana.
ReplyDeleteProtas-Iringa
hakuna kiongozi anaemshtumu Nsajigwa ila kuna washabiki wanaomshutumu Nsajigwa. Mi nimemuunga mkono nSAJIGWA. nI JAMBO LA bUSARA...KWANI KAMA KOCHA unafanya analysis unaona mambo yanvyoenda na unaangalia uwezo wako...unaachia ngazi
ReplyDeleteMbona mnasema tu aliachia ngazi siku moja baada ya kuondolewa ktk michuano ya sportpesa hamja tupa wasifa wake jinsi alivyofanikiwa akiwa kama kocha yanga, hamja break down kashinda match ngapi, kadroo ngapi na amefungwa ngapi..nasikia ana droo chache kuliko match za ushindi na kufungwa ila ameongoza kufungwa zaidi kuliko kudroo na kushinda etiii toka azaliwe hajawahi ongoza yanga kwa ukocha akashinda pia nasikia match alizoongoza yanga ikashinda ni zile za mazoezini wakicheza yanga A na yanga B...siyo mimi jamani natumia records zao maana sasa hivi yanga ni wazee wa records ukishangilia ushindi utasikia tulishachua mara tatu..sasa kwa kutumia mfumo huo wa records tunaomba wa-confirm.
ReplyDelete:d :d :-d :-d (o) (o)
ReplyDeleteMficha uchi hazai..
ReplyDelete..tatizo ni kubwa lakini wanachama hawashirikishwi katika kutatua....sasa ngome inaendelea kumeguka kocha, viongozi, wachezaji kutosajili...
Kumbukeni bado kuna mashindano ya CAF mechi kama nne zimebaki....lazima mfanye uchaguzi ndani ya wiki mbili, pia mteue benchi la ufundi la muda, na msajili wachezaji sio kuongea tu...lugha kama hizi hazitakiwi.
..tuko kwenye mpango, tunategemea, tunatafuta, tunaandika barua.....huu ni uzembe....wengine wanatoa pesa wanachukua mchezaji!
Mficha uchi hazai..
ReplyDelete..tatizo ni kubwa lakini wanachama hawashirikishwi katika kutatua....sasa ngome inaendelea kumeguka kocha, viongozi, wachezaji kutosajili...
Kumbukeni bado kuna mashindano ya CAF mechi kama nne zimebaki....lazima mfanye uchaguzi ndani ya wiki mbili, pia mteue benchi la ufundi la muda, na msajili wachezaji sio kuongea tu...lugha kama hizi hazitakiwi.
..tuko kwenye mpango, tunategemea, tunatafuta, tunaandika barua.....huu ni uzembe....wengine wanatoa pesa wanachukua mchezaji!
Makocha mara nyingi wanaajiriwa ili wafukuzwe Nsajigwa amefanya kazi kubwa katika mazingira Magumu lakini hakukata tamaa. Tusimlaumu kwa hatua aliyechukua, namshauri akasome apate daraja la juu la uko cha aongeze cv.
ReplyDelete