Mchezaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, ametoa maoni yake kuhuiana na mwenendo wa timu hiyo namna unavyokwenda hivi sasa.
Chambua ameamua kufugunguka kutokana na Yanga kuwa na mwendelezo mbaya tangu kuondoka kwa Kocha Mzambia, George Lwandamina, akieleza inabidi kikosi inabidi kifumuliwe upya.
Mchezaji huyo wa zamani ameeleza kuwa Yanga ina tatizo katika idara ya Golikipa hivyo ni vema likafanyiwa mabadiliko mapema wakati ambao ipo katika mashindano ya kimataifa.
Vievile Chambua amesema Yanga inatakiwa ifanyiwe mabadiliko ya wachezaji ipate wenye ubunifu na ufundi zaidi, tofauti na waliopo hivi sasa aliowaeleza kuwa wameshindwa kuisaidia Yanga.
Kauli ya Chambua imekuja kufuatia Yanga kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Kakamega HomeBoyz katika mashindano ya SportPesa Super CUP kwenye Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment