June 4, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, ameondoka usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9 kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Ngoma aliyesajiliwa na Azam kutoka Yanga, amesafirishwa kuelekea jiji la Cape Town ili kupata vipimo vya afya ili kuona tatizo lipi linalomsumbua.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa Azam FC, Jaffar Maganga, amesema kuwa watakuwa tayari kumgharamikia Ngoma endapo itabainika ana tatizo katika afya yake na kama atakuwa yuko sawa atarejea nyumbani.

"Kama Ngoma atabainika ana tatizo lolote katika mwili wake, klabu ya Azam itawajibika kutumia gharama zozote zile kwa ajili ya matibabu yake. Na kama ikitokea yuko sawa, atarejea nchini" alisema.

Ikumbukwe Ngoma wakati akiwa Yanga hakucheza takribani msimu mzima wa 2017/18 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, hivyo ilisababisha asionekane Uwanjani kwa muda mrefu.

Ngoma ambaye ni raia wa Zimbambwe, alisajiliwa na Azam kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ambapo alijiunga na Yanga kutokea FC Platnumz ya nchini kwao mwaka 2015.


1 COMMENTS:

  1. Narudia kuzipongeza klabu za Azam na Simba kwa kujali afya za wachezaji wao kwa mara kwa mara kuchukua hatua ya kuwatibia nje ya nchi wachezaji pale ambapo imeshindikana kwenye hospitali zetu hapa nchini. Simba wamewapeka wachezaji wao India. Azam wamewapeleka wachezaji wao Afrika Kusini. Hilo ni jambo jema sana na Mwenyezi Mungu atawaongezea baraka viongozi wenu wanaofanya maamuzi haya ya utu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic