June 13, 2018


Straika hatari wa Atletico de Madrid, Antoine Griezmann, amesema kuwa tayari ameshafikia mwafaka wa wapi atakuwa msimu ujao lakini akishindwa kupataja.

Kwa mujibu wa Sky Sports, wameeleza kuwa mchezaji amekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na klabu za Manchester United na FC. Barcelona ambao wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili.

Tangu msimu wa ligi kuu Spain ukiwa haujamalizika kumekuwa na taarifa nyingi za nyota huyo tegemo wa Atletico kuhusishwa kujiunga na Barcelona.

"Ni kweli tayari nimeshanya maamuzi yangu, lakini si muda mwafaka wa kueleza nitaenda wapi," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic