June 13, 2018


Uongozi wa klabu ya Monaco umefikia makubalino ya awali na Atletico de Madrid ya kumuuza mchezaji wake winga, Thomas Lemar.

Mchezaji huyo alikuwa anawindwa na klabu za Arsenal na Liverpool lakini kuna dalili kubwa anaweza akatimkia nchini Spain msimu ujao kujiunga na Atletico baada ya mazungumzo kwenda vizuri.

Lemar kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa huko Urusi na ingewezekana tayari angekuwa ameshasajiliwa kujiunga na Atletico mapema kabla ya michuano hiyo kuanza.

Ufaransa itaanza kibarua chake cha kwanza dhidi ya Australia Jumamosi ya wiki hii.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV