June 17, 2018




Pamoja na kufanya usajili ndani na nje ya Tanzania, jambo la kwanza ambalo watalifanya Simba ni kuangalia wale wenye msaada zaidi katika michuano ya kimataifa.

Simba wamejipanga kupata wachezaji ambao wanaweza kuifikisha mbali katika michuano ya kimataifa.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza, katika mjadala wa suala la usajili, zaidi linaangaliwa suala hilo.

"Unajua kama wachezaji wa kucheza ligi tayari tunao. Sasa zaidi ni michuano ya kimataifa," kilieleza chanzo.

"Hata kama ni mchezaji wa hapa nyumbani, basi awe ambaye tunaamini ana nafasi ya kutusaidia katika michuano ya kimataifa kwa uzoefu au uwezo."

Tayari Simba imeanza usajili lakini mambo yamekuwa yakienda kimyakimya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic