June 17, 2018



MWANDIKA, KOCHA MSAIDIZI WA YANGA.


Na Fahad Ally
Mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Yanga wameanza kukusanya fedha taratibu ili kukamilisha masuala kadhaa ya usajili.

Yanga inakabiriwa na ukata na imeelezwa, kuna fedha zimekuwa zikikusanywa na wadau mbalimbali lakini kimyakimya.

"Hali si nzuri na lazima tukubali, hivyo tunakusanya fedha kwanza," alieleza mmoja wa wajumbe wa kamati maalum inayoongozwa na Abbas Tarimba.

"Bila fedha hatuwezi kufanya kitu. Unajua Yanga ina madeni ya wachezaji mishahara na fedha za usajili ambazo hawajalipwa.

"Baada ya hapo ndiyo kuna suala mikataba mipya. Ni kazi ngumu sana na watu wafanye subira," alieleza.

Mambo ya usajili upande wa Yanga yanaonekana bado hayajatulia. Na kamati hiyo ya Tarimba iliyopitishwa na wanachama ndiyo inayohaha kujaribu kuweka mambo sawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic