June 17, 2018




Na Fahad Ally
Gor Mahia imeamua kutumia kikosi cha pili katika michuano ya Kombe la Kagame.

Michuano ya Kagame imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Gor Mahia, Dylan Kerr ameiambia SALEHJEMBE kwamba atatua Dar es Salaam na kikosi cha pili.

“Nitachukua wachezaji wa kikosi cha pili na wale ambao wamekuwa hawachezi.

“Unajua tuna mashindano mengi, zaidi ya mashindano matatu tofauti na wachezaji lazima ujue wanahitaji kupumzika.

“Hivyo watakoakuja, watapata nafasi ya kucheza na tutaona wachezaji wengine pia wanaoweza kutusaidia baadaye,” alisema.

Gor Mahia ambao ni mabingwa wa Kenya wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na hivi karibuni waliibuka wabingwa wa Kombe la SportPesa Super Cup.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic