June 28, 2018




Kuwa na kadi nyingi zaidi za njano ndiko kulikoing’oa Senegal katika mashindano ya Kombe la Dunia.

Katika kundi lao, Colombia iliyoifunga Senegal bao 1-0 leo pamoja na Japan zimefuzu hatua ya 16 Bora.

Senegal na Japan ziko sawa kwa pointi, mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kuifanya kanuni ya michuano hiyo kwenda katika suala la Fair Play ambalo kinachoangaliwa ni wingi wa kadi.

Kadi 6 za njano za Senegal zimekuwa nyingi kuliko zile za Japan wenye kadi nne tu. Maana yake, Senegal inakuwa timu ya tano ya Afrika kuishia katika makundi.

Maana yake, hakuna hata timu moja ya Afrika ambayo imevuka katika hatua hiyo ya makundi.

Waliolambwa kadi hizo za njano sita ni Gueye, Mbaye Niang, Youssouf Sabaly, Cheikh Ndoye, Idrisa Gana na Salif Sane.

4 COMMENTS:

  1. Kanuni ya kipuuzi, isiyokuwa na hadhi ya kombe la dunia.

    Haki ni kupambana uwanjani tena. Kwa hao walioringana.

    ReplyDelete
  2. Kanuni ya kipuuzi, isiyokuwa na hadhi ya kombe la dunia.

    Haki ni kupambana uwanjani tena. Kwa hao walioringana.

    ReplyDelete
  3. Waliyataka wenyewe,walikuwa wana uwezo wa kuwafunga Japan lakini kama kawaida ya waafrika wakaleta mbwembwe za kijinga matokeo yake wakaambulia sare.
    Tatizo wachezaji wa Africa kucheza ligi za Ulaya wanaona ndio kilele cha mafanikio na kudharau hata kombe la dunia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic