June 19, 2017


Simba inaamini inaweza kumsajili Obrey Chirwa kutoka Yanga lakini kama tu atavunja mkataba wa kuitumikia timu yake hiyo.

Kuna taarifa kwamba Chirwa raia wa Zambia, ameandika barua kuvunja mkataba baada ya Yanga kushindwa kumlipa mshahara kwa miezi mitatu.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa nyingine kwamba Yanga ilichelewa lakini ilifanikiwa kuwalioa wachezaji wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wanawasiliana na wakala wa Chirwa.

“Kama atavunja mkataba tunaweza kuangalia hilo na mawasiliano na wakala wake yanaendelea,” alisema.

“Si Chirwa pekee, hata (Donald) Ngoma. Tunaona ni wakati mzuri wa kuzungumza na wakala wake na ikiwezekana basi tutamsajili,” alisema.


Hata hivyo, Mzimbabwe huyo mwishoni mwa msimu alionekana kuisumbua Yanga ingawa yeye amekuwa akisisitiza kuwa ni majeruhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV