April 24, 2019


Young African Sports Club ilianzishwa February 11.1935 ,ni zaidi ya miaka 84 imepita toka Club pendwa ya wananchi kinara wa kuchukua ubingwa ligi kuu mara 27 ilipoanzishwa.

Tanzania ikiwa na idadi ya jumla ya mikoa 31 na Wilaya zake 196 ,na jumla ya vyuo vikuu 71 Tanzania bara na visiwani ni wakati sahihi wa Yanga African Sports Club kutengeneza ,"Club Ambassador, " kila chuo kikuu na kila Wilaya.

Ni wakati wetu kuitengeneza Yanga, katika mfumo thabiti wa uwazi na uwajibikaji katika kuwashirikisha wawekezaji wakubwa ambao ndio mashabiki.

Ukweli ulio uchi bila nguo,Yanga African ,ndio timu yenye mashabiki wengi Tanzania kuliko timu yeyote ile ,sasa ni wakati sahihi wa kila mashabiki wa Yanga ,kuwekeza mahaba na mapenzi kwa timu pendwa katika kutoa support ili tuweze kuitawala ligi ya Tanzania bara tunavyotaka.

Tutakuwa na mfumo wa kuchukua wanafunzi bora darasani katika nafasi 10 ,ambao ni mashabiki wa Yanga na kuwapa nafasi ya kupiga picha na wachezaji wao wanaowapenda.

Ni muda sahihi wa kufanya mataendo ambayo yatuwezesha kuipeleka Yanga kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam Stock Exchange [DSE] na kuanza kupigania kufanya vyema kwenye soko la kimataifa.

Yanga ni dhehebu na mashabiki ndio waumini wa hili dhehebu bora lenye harufu ya ubingwa unao tamalaki Jangwani.

Yanga :Daima mbele nyuma Mwiko.

Na Dismas Ten

9 COMMENTS:

  1. Hizo ndio ndoto tamu za Ali Baba

    ReplyDelete
  2. Ongea kwa takwimu zenye ushahidi siyo porojo kama za mlevi

    ReplyDelete
  3. Huna statistics Mwandishi mbulula wewe.. Ondoa Uandishi wako wa kijinga

    ReplyDelete
  4. Michango imefikia milioni ngapi?Bakuli limejaa?

    ReplyDelete
  5. Ndoto zako hizo ni za alinacha za kuota mchana kweupe.Na umbumbu wako eti ataita wanafunzi 10 bora wawe wanapiga picha na wachezaji wanaowapenda ....sasa ili iweje?...hata hueleweki ni bora hata kumsikilza mzee wa liquid.

    ReplyDelete
  6. Yanga inahitaji msemaji mhamasishaji mwenye kujitambua sio huyu kilaza

    ReplyDelete
  7. Mm kipenzi cha yanga niseme ukwel nkahisi stori bado inaendelea from my heart sijapata connection ya kichwa cha habari ila n kwel yanga inawatu sema viongozi ni tatizo katika Management na planning siku mm et niko kiongozi taasisi kama yanga one year deal done

    ReplyDelete
  8. Yaani ni Vita kati ya Yanga vs TFF, Bodi ya Ligi, Waamuzi, Magazeti, Serikali....na maadui wengine.....sasa mechi ya Azam vs Yanga imehamishwa uwanja wa uhuru....YANGA NI IMARA....YANGA IMESIMAMA KIDETE YANGA INAJENGWA NA WANANCHI WASIOYUMBISHWA PAMOJA NA FITINA NA CHUKI LAKINI MWENYEZI YUKO UPANDE WAO........"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic