June 7, 2018

Juhudi za madaktari wa Simba zimefanikiwa na kipa namba moja, Aishi Manula ataanza leo.

Simba inaivaa Kakamega Homeboys katika mechi ya michuano ya SportPesa Super Cup, mechi ya nusu fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Afrah mjini Nakuru, leo.

Manula aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Sharks na kulikuwa na hofu ya kumkosa leo.

Hata hivyo, beki Yusuf Mlipili hataanza katika kikosi cha Simba leo kwa kuwa hakuwa fiti kwa kiwango sahihi baada ya kuumia mechi iliyopita.

Imeelezwa, Mfaransa Pierre Lechantre anaweza kumuweka Mlipili, benchi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV