June 7, 2018


Na George Mganga

Wakati klabu ya Simba ikielekea kutoa tunzo kwa wachezaji wake pamoja na viongozi waliofanya vizuri kwa msimu wa 2017/18 zinazojulikana kama Mo Simba Awards, Juni 11 2018, wachezaji wanaowania wameanza kutajwa.

Katika nafasi ya kipa bora, Aisha Manula, Said Nduda na Emmanuel Mseja ndiyo makipa waliotajwa kuwania nafasi hiyo.

Ukiachana na makipa, kwenye nafasi ya mabeki wahusika ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Yusuph Mlipili ndiyo wanaowania tunzo hiyo.

Leo pia Simba wametaja wachezaji wanaowania tunzo ya kiungo bora ambapo Shiza Kichuya, James Kotei na Jonas Mkude ndiyo waliopo kwenye kitengo hicho.

Mbali na wachezaji pamoja na viongozi, tunzo moja itaenda kwa shabiki bora aliyefanya vizuri zaidi kwa msimu wa 2017/18.

Hafla ya utoaji wa tunzo hizo itafanyika katika ukumbi wa hotel ya Hyatt Regency Hotel iliyopo jijini Dar es Salaam.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV