June 6, 2018



Na George Mganga

Baada ya kuenea uvumi kuhusiana na kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, kuelezwa kuwa anataka kuondoka klabuni hapo na baadaye akaibuka kukanusha uwepo wa taarifa hizo, Djuma amefafanua namna mahusiano yake na kocha mkuu, Pierre Lechantre namna yalivyo.

Wakati Djuma akiwasili Simba kuanza kukinoa kikosi hicho ikiwa ni mapema baada ya Joseph Omog kuondoka, alikiongoza kikosi huku akionekana kusimama kila wakati kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo dhidi ya timu pinzani ukiendelea.

Kumekuwa kunaelezwa kuwa kitendo cha kocha huyo kuacha kufanya hivyo kwa mechi za hivi karibuni hivi kuwa ni ishara ya kutokuelewana na Mfaransa, Lechantre.

Kutokana na kuelezwa kwa tetesi hizo, Djuma amefunguka na kusema kutokuelewana kazini ni jambo la kawaida na haina maana kwamba kunakuwa na ugomvi ambao unaweza sababisha kufanya maamuzi ambayo si sahihi.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Kocha huyo Mrundi amefafanua kitendo chake cha kuacha kusimama kwenye benchi la ufundi wakati mchezo ukiendelea kama ilivyokuwa zamani, haina uhusiano wowote na mahusiano mabaya na Lechantre kama wengi wanavyodai.

Djuma ameeleza kuwa yeye bado yupo Simba na ataendelea kuwepo mpaka pale mkataba wake utakapomalizika.

Ikumbukwe Djuma alipowasili Simba alitia kandarasi ya miaka miwili hivyo bado kibarua chake hakijafikia ukingoni.

3 COMMENTS:

  1. Jamani watu waungwana hawasemi kila kitu lakini maelezo ya Djuma ni kwamba lipo tatizo pale na ndio maana ushindi wa sasa wa Simba ni goli la bahatibahati. Wachezaji wanacheza kama wapo mazoezini muda mwingi ni kudefend wanapack bus. Yasemwayo yapo kama hayapo basi yanakuja. Viongozi wa Simba msidharau jambo hili likiachiwa litaharibu timu. Ni kweli Djuma haonekani akiwahamasisha wachezaji wake kama zamani. Hii nini? Lazima makocha waelewane. Djuma ni kocha mzuri tunamuhitaji. Waelewane tusonge mbele.

    ReplyDelete
  2. Masoud Djuma kaacha kusimama wakati wa mechi ni kutokana na vidomodomo na miguno ya baadhi ya watu wanaojiita waaandishi au watu wa mpira kumsema vibaya kuwa hupaswi kusimama kwani yeye sio kocha mkuu. Lawama hizo zilielekezwa kwa kocha msaifizi wa Yanaga vile vile Shadrack Msajungwa.
    Mimi Watanzania nawafananisha na kisa cha bwana alieamua kufunga safari yeye na mwanae kwa kutumia usafiri wa Punda. Mwanzo wa safari yao aliamua yeye na mwanae kujipakiza kwenye punda wao na kuanza safari yao lakini muda si mrefu baada kupishana na baadhi ya watu walilani kitendo cha kuona punda kabeba watu wawili kwa madai yakwamba binaadamu wamekuwa wakatili kiasi cha kutisha na baada ya kusikia malalamiko ya watu wale juu ya uonevu wanaomfanyia punda basi bwana msafiri akaona isiwe shida hivyo akamuamuru nwanae wateremke kutoka kwenye mgongo wa punda na kuamua kufanya jitihada na juhudi za kumbeba punda badala yake na kuendelea na safari yao ili kuuhidhirishia umma kuwa wao ni watu wenye mapenzi na wanyama kupindukia tofauti na wanavyosemwa lakini maamuzi yao ya kumbeba punda yalionekana ni kituko na watu huku wakihoji kwa kejeli kama punda huyo alikuwa mgonjwa? Kusikia vile yule mzee akaona hii sasa ni dharau kwa usafiri wao kushukiwa kuwa ni mbovu ndipo walipoamua kutumia usafiri wao huo wa punda tena kwa baba kubakia kuendelea kutumia usafiri huo wa punda na kumuamuru mwanae kutembea kwa miguu lakini baada ya kupishana na kundi la watu walishangazwa sana na kulaani kitendo cha yule mzee cha kumuacha mwanae atembee kwa miguu wakati yeye mwenyewe akiinjoyi usafiri wa punda na kama vile haitoshi watu wale walifika mbali kwa kusema wazee wa sasa hawana mapenzi na watoto wao, basi yule mzee kusikia zile shutuma akaona isiwe shida wacha aonyeshe mapenzi yake kwa mwanae hivyo akaamua kuteremka kutoka kwenye mgongo wa punda na kumpandisha mwanae ili aendelee kutumia usafiri ule wa punda na kuendelea na safari yao lakini cha kushangaza tena baada ya muda si mrefu ya kuendelea na safari yao walikutana na watu amabao walikerwa sana na kitendo cha mtoto kumuacha baba yake atembee kwa miguu huku yeye akiwa juu ya punda kwa madai yakuwa watoto wa sasa wamekosa adabu na malezi na kutokuwa na huruma juu ya wazee wao basi yule mzee kusikia zile lawama tena akaona isiwe shida hata kidogo akamtaka mwnae ateremke kutoka kwenye mgongo wa punda na kuamua wote kutwmembea kwa miguu huku wakiamabta na punda wao na kuendelea na safari yao lakini tena baada ya kupishana na baadhi ya watu wishtushwa na kitendo cha mtoto na baba baada ya kuwaona wakitembea kwa miguu wakati usafiri wanao. Watu hao walifika mbali zaidi kwa kumtuhumu baba na mwanae kuwa na ukosefu wa akili ndipo yule mzee alipoona enough is enough na kunena na mwanae ni wakati wa kuchukua maamuzi yao binafsi ili kukamilisha safari yao la sivyo wakisiza ya watu hawatafika wanapotaka kwenda ndipo walipochukua maamuzi ya kujipakiza tena kwenye punda wao na kutimua vumbi kuendelea na safari yao. Ukitaka kufanya lako katika jamii ya kitanzania basi fanya ila tarajia kusikia wajuaji na kelele za kila aina za kukuelekeza na kukuponda lakini cha kufanya wewe ni kuendelea na kukamilisha ulichokuwa unataka kukifanaya na achana kusikiza na kuyumbishwa na kelele za watu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli bro, niliwasikia sana hao waandishi unafki. Sasa kutosimama imekuwa kesi tena

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic