June 6, 2018


Wakati taarifa zikielezwa kuwa Simba wapo kwenye mazungumzo na kiungo wake, Said Ndemla ili kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea, watani zao wa jadi wanahusishwa kutaka saini ya mchezaji huyo.

Ndemla hajawa sehemu ya kikosi cha kwanza katika msimu wa 2017/18 na badala yake alikuwa akianzia benchi kwa takribani mechi zote ambazo wekundu hao wa Msimbazi wamecheza msimu uliomalizika.

Taarifa zinaelezwa kuwa Yanga wameanza mazungumzo naye kwa ajili ya kumsajili ili kwenda kuboresha safu yao ya kiungo ambayo haifanyi vema kwa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Ndemla ameshamaliza mkataba ndani ya Simba lakini vilevile inaelezwa kuwa uongozi wa klabu yake umeanza mazungumzo naye kwa ajili ya kuongeza mwingine.

Endapo Ndemla atajiunga na Yanga atakuwa anaungana na aliyekuwa mchezaji mwenzake, Ibrahim Ajibu aliyeondoka Simba kabla ya msimwa 2017/18 kuanza.




8 COMMENTS:

  1. Waandishi nyie ni wachonganishi sana

    ReplyDelete
  2. Kweli waandishi wamichezo wengi wabongo ni wapotoshaji unakuta sisi ambao tunategemea habari kwao tunajuwa kuliko wao wenye fani yao...wamekaa kuaharibiana hawana heshima na fani yao.,yaani taharifa za vijiweni wanazileta kwenye mitandao...

    ReplyDelete
  3. Naende nae akapambane na mgomo wa kutokulipwa mishahara

    ReplyDelete
  4. Mwandishi ni Simba kwa hiyo anaandika hivyo ili Simba waarakishe kumsajili

    ReplyDelete
  5. Kweli uandishi wa aina hii ni wa hovyo labda ameahidiwa kitu kidogo na wakala wa mchezaji fulani kutia pressure mchezaji wake kuingizwa kwenye kandarasi hivyo utaona muandishi anachapisha habari za uzushi.

    ReplyDelete
  6. Sasa hivi naona fani ya uandishi imeingiliwa na uongo....sijui kwanini, inabidi sheria kali iwepo kuwafutia leseni waandishi waongo na wachonganishi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic