June 19, 2018




Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola anaamini watakuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri zaidi msimu ujao.

Matola amesema watakuwa wakifanya usajili wao bila mbwembwe kwa ajili ya kuongeza wachezaji wanaowataka.

“Tunajua wapi na wapi tunahitaji kuongeza nguvu au kuziba mapengo. Lakini halitakuwa jambo la kutangaza kila jambo,” alisema.

Matola amesema kikosi chake bado kilikuwa imara na sehemu kadhaa tayari amezianisha kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri wakati wa usajili.

Lipuli zilikuwa kati ya timu ambazo zilijihakikishia kubaki Ligi Kuu Bara baada ya kuwa zimerejea.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic