June 19, 2018




Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera anatarajia kurejea nchini Jumamosi hii.

Kocha huyo alikuwa kwao nchini DR Congo ambako alikwenda mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu.

Zahera atareja nchini tayari kuanza kazi ya kukinoa kikosi chake kujiandaa na mechi yao ya tatu ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Mara baada ya kurejea nchini mara moja Yanga wataanza mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Yanga inatarajiwa kuivaa Gor Mahia katika mechi ya Kombe la Shirikisho JUlai 18 mjini Nairobi, Kenya.

Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidhi Saleh amethibitisha kwamba mara baada ya kurejea kwa kocha wataanza kujifua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic