June 1, 2018


Wakati vuguvugu la usajili wa awali likiendelea kuteka vichwa vya wadau wa soka nchini, uongozi wa Yanga umefunguka kuhusiana na baadhi ya klabu zinazosajili kupitia mlango wa uwani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa kuna baadhi ya klabu 'hajazitaja' zimekuwa zikisajili wachezaji pale wao wanapowataja.

Kutokana na vitendo hivyo kusubiri Yanga itaje wachezaji ilio kwenye mipango nao kisha timu zingine zinaibuka na kuwasajili, Mkwasa amesema kuwa huo ni usajili wa uwani unaoonesha mapungufu kwa wapinzani.

Mkwasa amefunguka kwa kusema kuwa hilo linaonesha kuwa namna gani Yanga ina kiwango kikubwa cha kuchagua wachezaji tofauti na klabu zingine ambazo zimekuwa zikisubiri wataje majina kisha ziwakimbilie kuwachukua.

"Unajua kuna klabu zimekuwa zikisubiri sisi tutaje majina kisha zikimbilie kuwasajili, hilo linaonesha namna gani sisi tunakuwa na uwezo mkubwa wa kuuchagua wachezaji tofauti na wanaowasajili kupitia mlango wa uwani" amesema Mkwasa.

8 COMMENTS:

  1. Uwezo unaotakiwa ni uwezo wa kulisaskata soca uwanjani na kupata ushindi sio uwezo Unaweza ukachaua mwanamke mzuri lakini huna uwezo wa kumuoa, hapo unajisifu nini. Nanyi wakati wenu si vilevile mkiwangoja Simba wamechaguwa na baada ya muda kutokana na uwezo mliokuwa nao wakati ule mkawa mnawachukuwa amba baadhi mnao mpaka leo. Au si keeli?

    ReplyDelete
  2. Mkwasa kama fala umesahau Simba walivyokuwa wakitaja wachezaji wake alafu nyinyi kesho yake mnawatia sumu..kama huna kumbu kumbu hizo mulize Bin Kleb anaweza akawa anakumbu kumbu nzuri kuliko wewe, Mlishawahi kulimliza Mzee Aden Rage kwa issue ya Mbuyu Twite, Issue siyo kwamba mnaviwango kuchagua wachezaji issue ni kwamba mnataka alafu hela hamna hiyo ni sawa unamtongoza demu mzuri alafu huna nguvu za kiume mwenye nguvu zao wanakuja kumnyoosha unabaki unalia ooh mimi nipo bora kwasababu najuwa kupoint watoto wazuri...mamake mtalia sana mwaka huu alafu mwenyekiti mwenyewe ndo huyo Akili Mali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Namimi nilitaka kumkumbusha hiliohilo. Ama kweli viongozi tunao hata wanayosema hayana mantiki.

      Delete
  3. Mkwasa na busara zako unaongea nini? Kwani kusajili ni kusajili, kutaja unamsajili nani na hujamlipa na kufanya naye mazungumzo ni uhuni. Tuchukue mfano wa Salamba mlisema mnataka kumuomba na wenzenu wamesajili sasa unalalamika nini? Hivi kweli mchezaji aje ajitolee kwenye timu yako, wakati wadhamini wanakupeni fedha kwani msisajili mnaanza kupiga kelele, Mkwasa ni kiongozi acha kulalamika bwana. Yanga haijafikia hatua ya kutia huruma kiasi hicho.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkwasa anaidhalalisha sana Yanga kwa kulalama tuuu tafuta ufumbuzi wa matatizo ya klabu na wachezaji acha kulalama tuuu

      Delete
  4. Kumbukumbu zinaonesha..Aden Rage hakulizwa ila alijiliza mwenyewe. Wachezaji wanachagua wenyewe wapi pa kwenda...Simba SC haijawahi kuteteleka kiuwezo kutokana na uwepo wa Friends of Simba chini ya Hans Pop, Kabulu na Aveva. Walipigana mwanzo mwisho. Rage alitaka kupita shortcut kwa kumsajili Twite kupitia APR wakati Twite hakuwa mchezaji wa APR. Kama kumbukumbu zako zipo sawa...Yanga walitaka kumsajili Mbuyi Twite na Kabange Twite kwa pamoja na ni baada ya michuano ya Kagame iliyofanyika Dar. Rage akasafiri kwenda Ruanda kufanya mpango bila kujua kuwa mchezaji yupo APR kwa mkopo. Bin Kleb yeye alienda Kongo kwenye timu ya Twite. Nani sasa alitaka kufanya uhuni?????Business competition ipo juu....hata Uingereza, Spain, France na Italy mambo yapo hivyo.

    Mpira wa Tanzania tunakwenda kwa kukomoana..yeye asipate na mimi nipate. Usajili ni Sayansi lakini pia ni Art. Nina maana ili ufanye usajili ni lazima uangalie matakwa ya Benchi la ufundi. Mwisho wa siku utamjazia kocha wachezaji wote wa eneo moja...Nikukumbushe....Omog alisema "kuna wachezaji wengi walikuwa si chaguo lake"...angalia kwa sasa....unae Okwi, Bocco, Salamba, Kaheza na wengine na bado kocha anataka striker mwenye akili wa kucheza pale mbele wa nje. Pesa sio kigezo cha kuwa na wachezaji wazuri...ila mahitaji ndio yatakufanya uwe na uwezo wa timu bora. Wachezaji wanaocheza ndani ni 11 na si 20. Utasajili wengi lakini hawa wengine ili wapate nafasi inawalazimu wasubili na kuwaombea wengine waumie. Bado timu itaendesha kwa mfumo uleule wa mwaka huu...ndio maana striking force ya Blagnon, Mavugo na Ajib imepitwa pointi moja na striking force ya Bocco, Kichuya na Okwi.Kumbe mwaka jana hawakuwa wabovu ila timu nyingine nazo zilikuwa imara.

    Kwa imani aliyokuwa nayo Mo..katika sajili zake..naamini atasajili wachezaji wengi bila kufata matakwa...sana ni wale wanaotajwa. Mo anaumia kuona fulani anakwenda huku....nae atamtaka. Ngoja tuone atakachotaka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Issue hapa ni nini? ???? haieleweki

      Delete
  5. Mchezaji akigoma anasema ana mststixo ya familia au mgonjwa na akionekana husema sasa yupo fiti

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic