MFARANSA LECHANTRE ASEPA ZAKE KWAO AKIWA AMEKAA MIEZI SITA BONGO
Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre jana ameondoka nchini kuelekea kwao Ufaransa baada ya kumalizana na mabosi wa Simba.
Mfaransa huyo alikuja kuchukua nafasi ya Mcameroon Joseph Omog ambaye alifukuzwa kazi kutokana na mabosi wa klabu hiyo kushindwa kuridhishwa na kiwango.
Lechantre amerejea kwao baada ya mabosi wa Simba kugoma kumuongezea mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Kocha huyo alisaini mkataba wa miezi sita pekee ambayo imemalizika mwezi huu ambapo ilifika hatua akasusia kukiongoza kikosi chake kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya kwa kuamua kukaa jukwaani.
Kocha Msaidizi, Masoud Djuma amebaki na kikosi kwa sasa huku ikielezwa kuwa Suleiman Matola anaweza akaondoka Lipuli kuja kusaidiana na Djuma ambaye inaelezwa inawezekana akapewa Ukocha Mkuu.
Hakuna ubishi ni kocha mkubwa lakini wa bajeti kubwa vile vile. Kocha ambae alishazungukia mara kadhaa viunga vya waraabu nchi kama Qatar si mtu wa mchezo mchezo kuingia nae kandarasi na ndipo ninaposema Mo na SIMBA yake hivi sasa sio timu ya mchezo mchezo . Kumuajiri yule mfaransa japo kwa wiki moja kunahitaji ujasiri wa hali.lakini kitendo cha simba kumalizana nae bila ya mikwaruzano yeyote kuhusu stahiki zake ni jambo la kuipongeza Simba na uongozi wake. Kama usemi unaosema kocha huajiriwa kwa ajili ya kufukuzwa kazi lakini Lechnte hakufukuzwa kazi mkataba umeisha na Simba inaonekana kutorishwa na huduma yake kutokana na sababu wanazozijua wao hivyo waandishi lazima mtofaushishe kati ya kocha kumaliza makataba na kukatishwa mkataba.
ReplyDeleteHongera ndugu yangu kwa kuwapa somo waandishi wetu. Ila hawasikii. Utaona kesho wataandika Simba imeendeleza tabia yao ya kafukuza makocha. Huwa nawashangaa. Kwani mtu si anaajiri anayemtaka, akiamua basi akamlipa stahiki zake zote, kosa lipo wapi????
DeleteSasa kweli Simba imeingia kwenye soka la kibiashara na la kimataifa.Hii ndio professional football.Upande wetu Yanga badala ya kuahangaika na mchakato wa mabadiliko lkn kuna wenzetu wanakodi dalaladala kwenda kumsujudia Manji arudi kuwa mwenyekiti wakati vyeo hivyo vimeshafutwa na Fifa.Najiuliza kama Simba imewachukua takrban miaka miwili kubadilisha mfumo dume kwenda mfumo wenye tija then sijui Yanga itatuchukua muda gani pengine miaka mitatu maana kwa stahili hii tunayoendelea nayo ya kumbembeleza mwenyekiti aliyeomba kujiuzulu basi bado ni mambumbu wa kupitiliza.Wakati wanachama wa Simba watakapokuwa wanagombea kununua hisa zao 51% sie Yanga tutahamasishana kutembeza bakuli ili tulipe mishahara ya makocha,wachezaji na watendaji wa klabu.Wakati wenzetu Simba wamemalizana vizuri na makocha wao wa awali walio achana nao kina Mayanga,Omogi, Leachantre ,Hibib lkn Lwandamina ameondoka akiwa hajamaliziwa mishahara.Bado tunataka kusajili wachezaji wa bei mbaya ili tu tuwakomoe Simba.sitashangaa yale yaliyotokea kwa Ngoma na Ajibu yakajirudia tena msimu huu.Muhimu ni kujipanga kwa mwaka mzima ili tuondokane na fikra mbovu kuwa bila Manji basi Yanga haiwezi kufanikiwa.Ni maoni yangu na uhitaji kutoa mapovu kunijibu.
ReplyDeleteMwandishi naye ana uhuru wa kuweka mitazamo yake bhana... nadhani suala la wengi wetu kukosoa waandishi ni kutafuta kiki tu kama vipi kasomeeni na ninyi... Suala la mitazamo binafsi lipo na ndio maana halisi ya uchambuzi so, mnataka achambue kama mnavyotaka ninyi?... watanzania acheni ushamba mwandishi hana kosa ili mwenye kosa ni wewe unayemuona si chochote kumbe we ndio zero zaidi, Nachukizwa sana na tabia za kishabiki zinazomlenga mwandishi!
ReplyDelete